Uchanguzi au Zoezi?

Je! Kuna uchaguzi au ni zoezi tuu ili kuhakikisha ya kuwa hatuendi kinyume na katiba? Hivi karibuni kaka zetu kutoka muungano wa Tanzania watakuwa na uchaguzi ili kuumua watampa nani uongozi wa taifa lao. Uchaguzi ni wa muhimu kwa kuwa kutokana na tukio hilo wanainchi wakawaida wanapata fursa ya kushiriki kwenye uongozi wa taifa lao, pia kutokana na tukio hilo wanapata fursa pia ya kumchagua wanae kisia ya kuwa atatimiza mahitaji yao ya kila siku na kuinua hali yao ya maisha ya sasa na ya vizazi vijavyo.


Cha kusikitisha ni kwamba kwa maoni yangu tukio la mwaka huu halistahili kuitwa uchanguzi. Kwa maana hakuna cha kuchangua ila ni zoezi la kumtewa ni nani bora zaidi kati ya Lowasa na Magufuli ambao wote ni wanachama wa CCM. Uchaguzi bora ni ule wenye upizani;kwa kuwa upizani inatupa fursa ya kuweza kusikia mawazo tofauti, sera mpya, viongozi wapya,na mwanzo mpya ili kuwezesha mabadiliko. Kwa kweli kati Lowasa au Magufuli hakuna atakaye leta mabadiliko ila itakuwa ni kuendelesha uongozi na sera za CCM ambazo kwa miaka 50  hakuna cha kujivunia.


Lowasa anaweza tutapeli ya kuwa hakubaliani na mpizani wake na yakuwa yeye nitofauti na Magufuli, na yakuwa ataleta maabadiliko tunayo hitaji  kwa haraka ila hivi majuzi tuu walikuwa wanakula na kunywa katika meza moja bila kuhofia nchi ilikuwa ikizama kutokana na uongozi duni.Zote tunaelewa ya kuwa wote wawili walikuwa ndani ya serikali na hawakufanya lolote kuleta mabadiliko, kupingana na ufisadi, kuzuia wizi ya mali ya umma, kuboresha maisha ya mtazania wa kawaida na chaga moto zingine zinazo wakumba watanzania wote.


Changa moto langu kwa watanzania wote,  ni kuwauliza mtakopo kuwa mnapo piga kura mwaka huu na takaka mujiulize fursa hii ya kuleta mabadiliko iliwapita vipi?Ni ukosefu wa upizani wenye mizizi imara?,Ni uoksefu ya viongozi wapya? , ni siasa mbaya?, au niwatanzania wengi kuto jihusisha na siasa?.


La mwisho nikuwatakia kila la heli mnapo mchagua ninani bora kati ya hao wawili na kutarajia mtakaye mchangua atatimaza ahadi zake kwenyu.

 

Hadi wakati mwingine kuweni na kampeni zisizo na furughu na uchaguzi bora.

Jirani Yenyu

Maasai

Post your comment

Name

Email

Message


MALAZI KENYA SAFARIS
HOME AWAY FROM HOME.
For All Your Travel Needs And Accomodation